
Ali Kiba aliwarusha warembo na washabiki wa Miss Tanzania EU Ujerumani Mwanamuziki wa kizazi kipya ambaye alipagawisha mashabiki kibao kutoka sehemu mbali mbali za Ulaya.
Ali kiba na vibao vyake vikali; Cinderella, Mac Muga, Nakshi nakshi nk. Viliwarusha washabiki toka mataifa mbali mbali usiku huo.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa Ngemera alifungua shindano hilo kwa kusisitiza waandaji wa shindano hilo kutoishia hapo bali liendelee tena na tena.
Katika ufunguzi wa shindano hilo ambalo lilidhaminiwa na shirika la ndege la Ethiopia, wimbo wa taifa uliimbwa na Godlove Muliahela mtanzania anayeimba Gospel jiji la Mülheim nchini Germany.
Maelezo na picha kwa wingi zaidi nenda www.malumbosjr.blogspot.com ambaye kaleta habari hizi na picha
No comments:
Post a Comment