Tuesday, July 1, 2008

FM ACADEMIA WAFUNIKA KILI 2007


Wanamuziki wa bendi ya FM Academia a.k.a Waze wa ngwasuma, wakitumbiza wakati wa utoaji wa tuzo za muziki za Kili 2007 katika ukumbi wa hoteli ya Kempinski,jini Dar hivi karibuni.

AY na Mwana FA Wa weka historia Tuzo ya Kili 2007


Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yessaya a.k.a AY (kulia) na Hamisi Mwinjuma 'Mwana FA' wakiwa na Tuzo ya Kili 2007 ya Wimbo Bora wa Kushirikiana wakati wa hafla ya tuzo hizo na wimbo ambao umewapatia ushindi wasanii hao ni ule uitwao ', Habari ndiyo hiyo'..Wadau pamoja na tuzo hizo kufanyika, lakini bado zimekuwa zikilalamikiwa mara kwa mara zifanyikapo,hasa wasanii na washabiki wenyewe kwamba zimekuwa zina kasoro,Je nini kifanyike katika kuziboresha tuzo hizi zenye hadhi ya Kitaifa?

MISS TANZANIA EU 2008 NI LUCY FUNDIKIRA July, 1, 2008


Pichani ni binti aitwaye Lucy Mwiza Fundikira ambaye hivi majuzi amejinyakulia taji la Miss Tanzania 2008 EU (nchi za Schengen).Shindano hilo lililofanyikia katika mji wa Essen nchini Ujerumani,lilipambwa pia na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya,Ali Kiba(kama inavyoonekana katika picha hapo chini) ambaye yupo ziarani katika nchi mbalimbali za Ulaya.
Lucy Fundikira ana umri wa miaka 18 na anaishi na wazazi wake katika mji wa Rotterdam nchini Uholanzi.Kwa picha na habari zaidi kuhusu tukio hilo bonyeza


MwanaFA UNAOA LINI…?



Kwa mila na taratibu za jamii nyingi,hususani zetu za kiafrika,kijana akifikia umri fulani huwa anategemewa kuoa.Ikitokea ukafikia umri ambao kila mwanajamii anakutegemea “kujipatia jiko” na ukawa hujafanya hivyo, hapo lazima ujiandae na swali;unaoa lini?Ukikutana na shangazi swali ni hilo hilo.Ukikutana na mjomba naye anasimamia hilo hilo.Jamii nzima inauliza,unaoa lini?
Sasa je ukiulizwa swali hilo huwa unajibu nini?Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya,Hamis Mwinjuma a.k.a MwanaFA a.k.a Binamu anakupa msaada wa majibu katika single yako mpya inayokwenda kwa jina Bado Nipo Nipo huku akiwa amemshirikisha Miss Universe Tanzania 2007,Flaviana Matata.
Bado Nipo Nipo imepikwa na producer Harmy B.Pia MwanaFA anapewa tough na vichwa vingine kama vile Ambwene Yesaya(AY),Alan,Jabiri,Shehe na mwanadada aitwaye Anna.
Usikilize wimbo Bado Nipo Nipo kwa kubonyeza player hapo chini.Ningependa sana kusikia majibu kutoka kwa kinadada walio single, ni kweli anayoyasema MwanaFA?

warembo kukosha magari kwa hisani




Bonanza hili litafanyika leaders club Julai 5, 2008 ambapo warembo walioshiriki miss Tanzania kuanzia mwaka 1994 hadi sasa.Warembo hao wataosha magari ya watu mbalimbali kwa ajili ya kutunisha mfuko wa sickle cell foundation Tanzania.
Zoezi hili litadhaminiwa na Tigo, Le Grande Casino, Clouds 88.4 FM, Fleet & Fuel Technologies, Redds PremiumCold

Kampuni ya Mavazi Jita Wear ya Toa Nguo mpya!


Mkurugenzi wa Kampuni ya JITA Bw. Victor B inayo miliki Studio ya Jita Records,Radio Station City Sound Fm ambayo imesha anza majaribio mjini Dar pia Kampuni ya mavazi ambayo sasa inakuja kasi kwa ma vazi yake yenye nembo JITA WEAR nk kaa mkao mzuri kupata Quality ya mavazi yalio juu



sylvia ndiye miss Ilala 2008

mdau abdallah mrisho anatupasha kwamba Sylvia Mashuda ndiye Miss Ilala 2008 aliyefungua pazia la kuelekea Miss Tz mwaka huu usiku wa kuamkia leo pale Raiway Gerezani sasa ni City Garden Club. habari kamili bofya hapa

Shindano la Miss Tanzania EU 2008 MZUKA

Lucy (pichani akiwa na ali kiba) mwenye miaka 18 alishinda katika upinzani mkali na warembo wengine. Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Sabrina Bashir, ya pili na Jacquline Sabanya.
Ali Kiba aliwarusha warembo na washabiki wa Miss Tanzania EU Ujerumani Mwanamuziki wa kizazi kipya ambaye alipagawisha mashabiki kibao kutoka sehemu mbali mbali za Ulaya.
Ali kiba na vibao vyake vikali; Cinderella, Mac Muga, Nakshi nakshi nk. Viliwarusha washabiki toka mataifa mbali mbali usiku huo.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa Ngemera alifungua shindano hilo kwa kusisitiza waandaji wa shindano hilo kutoishia hapo bali liendelee tena na tena.
Katika ufunguzi wa shindano hilo ambalo lilidhaminiwa na shirika la ndege la Ethiopia, wimbo wa taifa uliimbwa na Godlove Muliahela mtanzania anayeimba Gospel jiji la Mülheim nchini Germany.
Maelezo na picha kwa wingi zaidi nenda www.malumbosjr.blogspot.com ambaye kaleta habari hizi na picha